Psalms 96

Mungu Mfalme Mkuu

(1 Nyakati 16:23-33)

1 aMwimbieni Bwana wimbo mpya;
mwimbieni Bwana dunia yote.
2 bMwimbieni Bwana, lisifuni jina lake;
tangazeni wokovu wake siku baada ya siku.
3 cTangazeni utukufu wake katikati ya mataifa,
matendo yake ya ajabu miongoni mwa mataifa yote.

4 dKwa kuwa Bwana ni mkuu mwenye kustahili kusifiwa kuliko wote;
yeye ni wa kuogopwa kuliko miungu yote.
5 eKwa maana miungu yote ya mataifa ni sanamu,
lakini Bwana aliziumba mbingu.
6 fFahari na enzi viko mbele yake;
nguvu na utukufu vimo patakatifu pake.

7 gMpeni Bwana, enyi jamaa za mataifa,
mpeni Bwana utukufu na nguvu.
8 hMpeni Bwana utukufu unaostahili jina lake;
leteni sadaka na mje katika nyua zake.
9 iMwabuduni Bwana katika uzuri wa utakatifu wake;
dunia yote na itetemeke mbele zake.

10 jKatikati ya mataifa semeni, “Bwana anatawala.”
Ulimwengu ameuweka imara, hauwezi kusogezwa;
atawahukumu watu kwa uadilifu.
11 kMbingu na zishangilie, nchi na ifurahi;
bahari na ivume, na vyote vilivyomo ndani yake;
12 lmashamba na yashangilie,
pamoja na vyote vilivyomo ndani yake.
Kisha miti yote ya msituni itaimba kwa furaha;
13 mitaimba mbele za Bwana kwa maana anakuja,
anakuja kuihukumu dunia.
Ataihukumu dunia kwa haki,
na mataifa katika kweli yake.
Copyright information for SwhNEN